Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WATEJA WA VODACOM SASA KUJICHAGULIA VIFURUSHI WAVITAKAVYO
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Katika dhamira yake ya kufanya ubunifu wa teknolojia kwa ajili ya kuwapeleka watanzania katika ulim...
Katika dhamira yake ya kufanya ubunifu wa teknolojia kwa ajili ya kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kwa kuwapatia huduma bora za kurahisisha maisha na kwa gharama nafuu leo, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua ofa mpya maalum kwa wateja wake inayojulikana kama ‘Ya kwako tu’ itakayowawezesha kujipatia vifurushi vya gharama nafuu kwa kadri ya matakwa yao wapendayo kuanzia vya huduma ya data, kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno.
Vodacom Tanzania
Mkurugenzi wa mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi ya huduma mpya ya ‘Ya kwako tu’ itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujipatia vifurushi vya gharama nafuu kadri ya matakwa yao wapendayo kuanzia vya huduma ya data, kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno. 

Ili mteja aweze kujiunga na huduma hii anatakiwa kupiga namba*149* 03# na kuchagua ya kwako tu, anayeshuhudia kushoto ni Afisa Mkuu wa Idara ya masoko wa kampuni hiyo, Ashutosh Tiwary na Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa kampuni hiyo, Danilo De Sousa

Akifafanua jinsi huduma hii inavyoweza kupatikana kwa wateja, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia amesema kuwa ofa hii inawezesha mteja kununua vifurushi kutokana na chaguo lake jinsi anavyotumia huduma za mawasiliano, kama anapendelea vifurushi vya muda wa maongezi anapatiwa, badala ya kulazimika kuingizwa kwenye vifurushi vya data na atakayehitaji kununua vifurushi vya data hatalazimika kununua muda wa maongezi kadhalika wanaohitaji vifurushi vya data na muda wa maongezi watapatiwa pia.

“Ofa hii ya Ya kwako tu imelenga kuleta unafuu kwa wateja wetu na kila mmoja atanufaika kwa kupata unafuu kadri ya matumizi yake na tunataka kuhakikisha kila mmoja anapata kifurushi kutokana na chaguo lake na huduma anayotaka na ndio maana Ofa hii ni kwa ajili ya wateja wenyewe kama ilivyo jina lake la “Ya kwako tu” yaani kwa ajili yako” alisema Mworia.

Alisema siku zote Vodacom inawathamini wateja wake na muda wote imekuwa ikisikiliza matakwa yao ili wapate huduma bora kadri wapendavyo na ndio maana imewaletea ofa hii yenye kuleta unafuu wakati huo huo kila mmoja akijipatia kirushi apendacho kwa kadri anavyopenda

“Tunatambua kuwa tunao wateja wa aina mbalimbali na tuko tayari kuwahudumia kulingana na matakwa ya kila mteja hii ina maana kuwa Ofa hii itawezesha kila mmoja kupata kifurushi cha huduma aipendayo tofauti na ilivokuwa awali ambapo wateja walikuwa wanaingizwa kwenye vifurushi bila kuzingatia matakwa yao ambapo wengine walikuwa wanapata huduma ambazo hawazihitaji ama kuzitumia kabisa,”alisema.

Ili kupata huduma ya ofa hii ya“Ya kwako tu” mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga simu namba*149* 03# ambapo katika orodha ya huduma kwenye menu ya simu zao kutatokea huduma ya “Ya kwako tu” ambayo itakuwa na orodha ya huduma anayohitaji kutumia.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top