Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: UFAFANUZI SAHIHI KUHUSU MAKATO YA ASILIMIA 18 KWENYE MIAMALA YA SIMU
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Kumekuwepo na sintofahamu kwa wananchi mara baada ya Waziri Fedha na Mipango Philip Mpango kuwasil...
Kumekuwepo na sintofahamu kwa wananchi mara baada ya Waziri Fedha na Mipango Philip Mpango kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2016-2017 na kueleza kuwa kutakuwepo makato ya kodi ya ushuru wa bidhaa katika miamala ya benki na simu za mkononi kwa Tozo ya asilimia 18%, Lindiyetu.com inakuletea ufafanuzi wa hiyo Tozo ili kukuondoa hofu ambapo leo ndio siku rasmi ya kuanza kwa tozo hiyo.
Philip Mpango
Makato ya tozo hiyo ni asilimia 10% + 18% ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) hivyo kuhusu makato kwenye kutuma na kupokea pesa na kutoa pesa kwa wakala inakumbukwa kuwa Kwenye hotuba ya waziri wa fedha na mipango alisema kuwa
"kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye ada zinazotozwa na watoa huduma wa simu katika kutuma na kupokea fedha badala ya ushuru huo kutozwa tu kwenye kutuma fedha pekee. Katika utaratibu wa sasa, baadhi ya kampuni zinazotoa huduma zimetumia mwanya kwa kuhamishia sehemu kubwa ya ada hizo kwenye kupokea fedha na hivyo kuwa nje ya wigo wa kodi.” Ambapo unapomtumia pesa mtu mfano shilingi 20,000 unakatwa kama Shilingi 500 huku Serikali inachukua kodi kwenye hiyo mia tano tu, wakati huo huo ukitumiwa kiasi cha pesa cha shilingi 20,000 ukienda kutoa kwa wakala itakatwa sh 1,200 ambapo kwenye hiyo 1,200 serikali ilikuwa haipati kitu.

Ndio maana Waziri Mpango katika hotuba yake ya kuwasilisha Bajeti alieleza kuwa "Katika utaratibu wa sasa, baadhi ya kampuni zinazotoa huduma zimetumia mwanya kwa kuhamishia sehemu kubwa ya ada hizo kwenye kupokea fedha na hivyo kuwa nje ya wigo wa kodi.”

Kwa kuzingatia kuwa serikali imekuwa ikipoteza mapato kwa mwanya huo wa ukwepaji kodi uliokuwa unatumiwa na makampuni ya simu kuongeza nguvu upande mwingine, hivyo utaratibu wa sasa serikali itachukua kodi ya 10% ya makato wakati unatuma pesa na kupokea pesa pamoja na VAT (18%), Ambapo ukiwa umetuma 20,000 na makato yakawa shilingi 500, serikali itachukua kodi ya asilimia 10% ya hiyo 500 ambayo ni shilingi 50, na pia itachukua VAT ambayo ni asilimia 18% ya hiyo 500, ambayo ni sawa na Shilingi 90, kwahiyo kwenye kutuma pesa, una katwa 500, kwenye hiyo 500, serikali inachukua (50+90=140)
Unapopokea pesa, ukaenda kutoa kwa wakala kwa mfano umetoa shilingi 20,000 unakatwa shilingi1,200. 

Serikali itachukua asilimia 10% ya hiyo 1,200. Yaani shilingi 120 huku VAT ambayo ni aslimia 18% ya 1200, ambayo ni shilingi 216 Kwahiyo, makato yanakuwa (216+120 =330).

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top