Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: TIMU YA CHELSEA YATANGAZA KUWATEMA WACHEZAJI WAKE WATATU.
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Chelsea fc imetangaza rasmi kuachana na wachezaji wake watatu waliokuwa wakiichezea timu h...
Timu ya Chelsea fc imetangaza rasmi kuachana na wachezaji wake watatu waliokuwa wakiichezea timu hiyo msimu uliopita.
Chelsea fc
Wachezaji hao walioachwa ni pamoja na Radamel Falcao aliyekuwa akicheza kwa mkopo akitokea timu ya FC Monaco, Alexandra Pato aliyesajiliwa mwezi Januari mwaka huu kwenye dirisha dogo akitokea Corinthians na kipa Marco Amelia aliyesajiliwa msimu uliopita kwa malengo ya kuchukuwa nafasi ya kipa namba moja wa timu hiyo Thibaut Courtois aliyekuwa majeruhi.

Tangu wajiunge na Chelsea, Pato na Falcao kila mmoja amefanikiwa kuifungia timu hiyo goli moja pekee huku Falcao akichezeshwa mechi 10 na Pato mechi 2. Aidha timu kadhaa kutoka ligi kuu ya Italia ikiwemo Napoli zimeonekana kuvutiwa na wachezaji hao huku wakitamani kuwasajili wachezaji hao.

Mpaka sasa timu ya Chelsea bado haijafanya usajili wa mchezaji yeyote huku kukiwa na tetesi za kuwafukuzia wachezaji kibao akiwemo Romelo Lukaku, Batshuayi na wengine wengi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top