Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: TEMBEA UJUIONEE...KUMBE BIKIRA NI MKOSI KWENYE HII JAMII
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa Hip Hop kutoka nchini Tanzania Darasa amewahi kuimba katika nyimbo yake ya Sikati Tamaa...
Msanii wa Hip Hop kutoka nchini Tanzania Darasa amewahi kuimba katika nyimbo yake ya Sikati Tamaa aliyomshirikisha mkali wa R&B Ben Pol mashairi yasemayo TEMBEA UJIONEE DUNIA IMEBEBA MENGI, akiwa na maana kubwa ya kuwa kwenye wengi kuna mengi, kinacho endelea nchini Malawi kinathibitisha kauli hiyo ya msanii Darasa kutokana na mengi na ya ajabu kwa tamaduni za mwafrika lakini huko Malawi ni jambo la kawaida.
Jackie-Appiah
Suala la Bikira kwa msichana ni heshima kubwa kwa familia husika ya binti huyo ambapo ni ishara ya malezi bora kwa kutunzwa vyema lakini nchini Malawi imekuwa tofauti ambapo wazazi huwa wanawalipa watu maarufu kama"Fisi” kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza, wakiwa na imani kuwa binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii.

Wazazi na jamii kwa jumla katika maeneo mengi ya kusini mwa Malawi wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka mingi "Fisi” ama wanaume wanaowabikiri watoto wakike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi, ambapo huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha kuwatembelea shangazi wake kabla ya kupelekwa kwa fisi, mafisi hulipwa takriban dola $7 sawa na shilingi 13,500.00 za kitanzania kwa kila kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka 11-14.

Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameeleza kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi "kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104” ”hiyo ndio tamaduni zetu”, ”Hapa mwanamke akifiwa lazima aje kwangu nimuondolee mkosi hata kabla ya kuzikwa kwa mumewe”, ”Mwanamke kabla kushiriki ngono na mwanamume mwengine lazima aje kwangu nimsafishe”. alisema Fisi huyo.

Aniva ambaye anaumri wa takriban miaka 40 ana wanawake wawili na watoto 5, Anasema kuwa pale anaposhiriki ngono na watoto hao huwa anapewa muda wa siku 3 hivi kumsafisha na kumuondolea mkosi Kulingana na tamaduni zao, ikiwa mwanamke ama binti anakataa asibikiriwe huwa wanaamini kuwa jamaa zao watafuatwa na mikosi na magonjwa.

CREDIT TO BBC SWAHILI

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top