Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: TAARIFA RASMI KUHUSU MBWANA SAMATTA KUTUA AS ROMA HII HAPA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Wakati suala la mshambuliaji Mbwana Samatta kuwa njiani kutua AS Roma ya Italia likiendelea kusam...
Wakati suala la mshambuliaji Mbwana Samatta kuwa njiani kutua AS Roma ya Italia likiendelea kusambaa mitandaoni, meneja wake amesema ni uzushi mtupu.
Mbwana Samatta
Jamal Kisongo ambaye ni meneja na mlezi wa Samatta, amesema hakuna lolote kuhusiana na hilo na Samatta anaendelea na maandalizi katika kikosi chake cha KRC Genk kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Ubelgiji. 
“Nimesikia pia, kuna watu kadhaa wameniuliza pia. Lakini ukweli ni hivi; Mbwana anaendelea na maandalizi ya Ligi Kuu Ubelgiji"
“Hakuna lolote kuhusiana na Roma hadi sasa labda kama litakuja baadaye Mawakala wake wote wanalijua hilo. “Timu haiwezi ikafanya mawasiliano ya kumuuza bila ya kuwaeleza mawakala wake, meneja wake. Ndiyo maana nasema labda suala hilo lije baadaye,” alisema Kisongo. 

Kuanzia leo asubuhi, taarifa za AS Roma ya Italia imekuwa kwenye mazungumzo Genk namna ya kumnasa Samatta ambaye ni nahodha wa taifa Stars, zimekuwa zikisambaa kwa kasi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top