Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: SIMBA YAENDELEA KUMKOMOA KESSY, YASEMA HAWAWEZI KUMRUHUSU KUCHEZEA YANGA, AVEVA ANENA HAYA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
YANGA imemuacha beki wake, Hassan Kessy katika safari ya Ghana kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shir...
YANGA imemuacha beki wake, Hassan Kessy katika safari ya Ghana kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Medeama. Sababu kubwa ni kutokamilika kwa taratibu za uhamisho kutoka klabu yake ya zamani, Simba kwenda Jangwani.
Hassan Kessy
Hata hivyo, Klabu ya Simba imesema haina lengo la kumkomoa mchezaji huyo wala watani wao Yanga, badala yake inataka kuona taratibu za usajili zinafuatwa.

Rais wa Simba Evans Aveva alisema itapeleka barua ya malalamiko Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) muda wa mchakato huo utakapofika.
Evans Aveva
Alisema Simba ina haki ya kupinga usajili wa Kessy kutokana na Yanga kuharakisha usajili, wakati mchezaji huyo bado hajamaliza mkataba Simba.
“Mkataba wa Kessy ulimalizika Juni 15 mwaka huu, lakini Yanga walimsainisha kabla ya muda. Taratibu za usajili hazitaki mambo kama hayo huo” alisema Aveva.

Alisema Simba hawawezi kumruhusu Kessy kucheza Yanga, ambayo haikufuata taratibu kama ilivyokwenda Mtibwa Sugar na kumsajili Andrew Vicent ‘Dante’.
Hassan Kessy
Kutokana na utata huo, Kessy ameshindwa kuitumikia Yanga katika mechi za hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.
Yanga itashuka dimbani Jumanne ijayo kucheza dhidi ya wenyeji wao, Medeama katika mchezo wa Kundi A.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top