Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: SHULE YA SEKONDARI LINDI YATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA JULAI 10, 2016 (+Picha & Video)
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Usiku wa kuamkia tarehe 10/7/2016 umekuwa ni wamajonzi kwa wakazi wa Lindi na Vitongoji vyake k...
ajali ya moto lindi sec
Usiku wa kuamkia tarehe 10/7/2016 umekuwa ni wamajonzi kwa wakazi wa Lindi na Vitongoji vyake kwa kutokea kwa tukio la Kuungua Moto Shule ya Sekondari ya Lindi.
ajali ya moto lindi sec
Mashuhuda wa Ajali hiyo wameeleza kuwa wanahisi chanzo cha ajali hiyo ni Hitilafu ya umeme.
Kikosi cha zimamoto kimelaumiwa na wadau mbali mbali kushindwa kutoa msaada wenyetija katika ajali hiyo na kusababisha Uharibifu huo kuwa mkubwa kwani gari la Zimamoto liliwahi kufika eneo la tukio lakini likishindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwani Mota ya kusukuma maji haikuwa ikifanya kazi hadi Kulazimu kutumia Gali za washa washa kusaidia kuzima moto huo.
ajali ya moto lindi sec
Moto huo umeweza Kuathiri Madarsa Tisa, Ofisi nne, Matundu ya Vyoo 24, Maabara Mbili pamoja na Chumba cha kufanyia Midahalo.
ajali ya moto lindi sec
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ilifika eneo la tukio na kujionea uharibifu huo uliosababishwa na Moto huo. 

TAZAMA VIDEO HII HAPA USHUHUDIE UHARIBIFU ULIOTOKEA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top