Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MKUU WA MKOA WA MTWARA KUWAONGOZA WANA MASASI SIKU YA USAFI JULAI 30, 2016.
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Siku ya usafi wa mazingira hufanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kote nchini ambapo kwa upande...
Siku ya usafi wa mazingira hufanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kote nchini ambapo kwa upande wa Halmashauri ya mji wa Masasi usafi utafanyika kimkoa siku ya tarehe 30/7/2016 kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 10:00 asubuhi.
Usafi Mji wa Masasi
Miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuongoza zoezi hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara atakayeambatana na wakuu wa Wilaya za mkoa wa Mtwara pamoja na wakurugenzi wa wilaya, Manispaa na miji mkoani humo.

Shughuli kubwa itakuwa ni kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo mbalimbali ya Mji kwa kushirikisha timu ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, viongozi mbalimbali ngazi za Wilaya, Halmashauri, kata, vijiji na mitaa ikiwa ni pamoja na wananchi wote wa Masasi.

Katika siku hiyo shughuli zote za kiofisi, kijamii na kibiashara zitasimama kipindi chote cha zoezi hilo ili kuruhusu wananchi wote kushiriki kikamilifu kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo yao.
Usafi Mji wa Masasi
Shughuli za usafi wa mazingira zitaanza rasmi tarehe 25/7/2016 na zitaendelea mpaka siku ya kilele yaani tarehe 30/7/2016 ambapo wananchi wote watafanya usafi kwenye maeneo yao ya makazi na biashara.

Kwa upande wa Halmashauri ya Mji wa Masasi tayari maandalizi yameshaanza ikiwa ni pamoja na kufanya uhamasishaji jamii kwa njia ya matangazo ya gari, Radio, Ujumbe mfupi wa simu za mkononi, matangazo ya mabango ya vitambaa yatakayowekwa kwenye njia kuu, kutoa matangazo kwenye nyumba za ibada pamoja na kuongea na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa.

Baadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa akiwemo Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Masasi na waheshimiwa madiwani wote wa jimbo la Masasi watashirikishwa kikamlifu katika kufanikisha zoezi hili la usafi wa mji wa Masasi lakini pia watu maarufu kwenye jamii na maafisa watendaji wa kata na mitaa wote watashiriki kuhamasisha jamii.
Usafi Mji wa Masasi


Ewe Mkazi wa mji wa Masasi jitokeze kufanya usafi pamoja na mkuu wa mkoa wa Mtwara siku ya tarehe 30/07/2016 kuanzia saa 12:00 Asubuhi hadi saa 4:00 Asubuhi.

kauli mbiu: “Ona aibu kuishi na uchafu, ifanye Masasi iwe safi”

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top