Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: LOWASSA:: NAINGIA IKULU KWEUPE 2020
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwaka jana, Edward L...
Aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwaka jana, Edward Lowassa, amesema njia ya yeye kuingia Ikulu ni nyeupe.
Lowassa
Lowassa amesema kuwa serikali ya Rais John Magufuli inarahisisha upinzani kushika dola kwenye uchaguzi mkuu ujao kutokana na kushindwa kuwatumikia wananchi vizuri.

Ametoa kauli hiyo Jumatano hii jijini Dar es Salaam wakati akifungua kikao cha kamati tendaji baraza la vijana la CHADEMA (BAVICHA).

“Hakuna anayependa maisha haya, kwa namna yeyote hakuna anayependa kushinda njaa. Maisha haya hakuna anayeyatamani,” alisema Lowassa.

Aidha aliongoeza kwa kusema, “CCM imewaonjesha maisha magumu watanzania, pesa imekuwa ngumu kupatikana.”

Kiongozi huyo pia amewapongeza vijana kwa kutii kauli ya Freeman Mbowe kutokuhudhuria kutokana na dhamira yao ya kutaka kuzuia mkutano wao unaotarajia kufanyika mjini Dodoma.

BY: EMILE MWAIPOPO

CHANZO: MWANAHALISI

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top