Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: HAMISA MOBETTO AZIJIBU TETESI ZA KUTAKA KUMPINDUA ZARI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Hamisa Mobetto yupo kwenye kitimoto. Mashabiki wa ‘first couple’ kama wanavyojiita wenyewe Zari na ...
Hamisa Mobetto yupo kwenye kitimoto. Mashabiki wa ‘first couple’ kama wanavyojiita wenyewe Zari na Diamond wamechukizwa na tetesi zinazoendelea kuvuma kuwa mrembo huyo ana uhusiano na muimbaji wa ‘Kidogo.’
Hamisa Mobetto
Kwa wale waliohudhuria sherehe ya birthday ya mama yake Diamond siku chache zilizopita, walidai kuwa palitaka kutokea timbwili baada ya Hamisa naye kuwepo kwenye sherehe hiyo iliyohudhuriwa pia na Mama Tiffah. Wanadai Zari hakupenda.

Hamisa alitumia Instagram kuzikanusha tetesi hizo.
“Binadaamu banaa. Now days U cant work with anyone wala kua close na yoyote just because unaogopa maneno yatakayo zuka after hiyo shughuli,” aliandika Hamisa kwenye picha akiwa na Bi. Sandra na dada yake Diamond, Esma.

“A birthday to remember 2016 #MamasBigDay ……. Na nshaanza kupokea emails za kazi ety haya kama unataka upendezeshwe na Hamisa mobeto ung’are sherehe yako iwee ya kuvutia kindly contact me kwa email ya apo kwenye Bio #HapaKaziTu Cc the boss @diamondplatnumz,” aliongeza.

Baadhi ya mashabiki hawakupendezwa na maelezo hayo na kuendelea kumrushia maneno.
“Jiheshmu we mdada sherehe sio yako umejipeleka mbele hadi kero kwani wengine hawakuepo.. vitu vingine vya kujiongeza tu @hamisamobetto Ona sasa kila siku ni wew tu skendo zakujitakia hizo,” ameandika mmoja.

“Kifupi umetia aibu sana hata kama wamekuzingiziaa lakini kwanin ulikubali kua chambo kiac hicho tatz liko wapi kama ungekaa 2 pembeni aya matuc yote yasingekukuta upande mwingne naumia kama moja wa fan wako lakin umeniangusha sana sna umekua kama tololi la familia ya mondi watu tunakuonea huruma mtot mdgo kama lulu amenyakua bebe baba wako kumbe huna lolot umeenda kututia aibu mtu sherehe c yako.. Kama ujui ile familia sio kabsa wao wamekutumia wew kama chambo leo matuc yote kwako.. Lea mtoto ako skendo hazikufai.”

Hata hivyo kwa upande wa Zari mambo yanaonekana kuwa mswano tu, walau kwa kile anachopost Instagram.
Zari
“Good nyt from the 1st family…. wishing all a blessed nyt. God bless,” aliandika jana kwenye picha hiyo juu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top