Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: BIFU LA JIKE SHUPA NA SHILOLE, NUH MZIWANDA AFUNGUKA HAYA HAPA, SIKILIZA AUDIO HII
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Kama wewe umezaliwa enzi za S.L.P nikitaja ngoma ya namba nane ya #Daz Baba sina shaka tuko pamoj...
Kama wewe umezaliwa enzi za S.L.P nikitaja ngoma ya namba nane ya #Daz Baba sina shaka tuko pamoja, lakini pia kwa wale wenzangu na mie wa .com ikitajwa #jikeshupa ya Nuh Mziwanda ama kichupa cha moto kabisa cha #matatizo alichodondosha jana Harmonize anayetokea lebo ya WCB nadhani tutakuwa tunakwenda sambamba.
Nuh Mziwanda
Sasa point ya msingi kwa leo sio hasa kuzizungumzia ngoma hizi bali mhusika aliyemo ndani ya ngoma hizi wakuitwa Zena maarufu kwa sasa kama Jike Shupa! Mrembo huyu mara baada ya kujizolea umaarufu mkubwa kupitia ngoma hii aliingia katika mzozo na X- Girlfriend wa Nuh yaani Shilole baada ya kujitapa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa ujumla kwamba yeye ni mzuri zaidi yake.

“Kwa kweli mimi namuona wa kawaida tu, akumbuke na mimi mzuri kuliko yeye na situmii mchina,” hayo ni maneno yake Zena maarufu kama Jike Shupa alipokuwa akizungumza kwa madaha na kumponda Shilole ambaye naye hivi karibuni aliwahi kusema yeye ndiye mwimbaji wa kike mrembo kuliko wote hapa Bongo.
Jike Shupa
Sasa baada ya mtifuano mkali baina ya wawili hao ulioendelea kurindima kwenye mitandao ya kijamii Nuh Mziwanda ambaye anadaiwa kuwa kwenye bifu zito mara dufu na Shilole baada ya kutoa Jike Shupa ameamua kufungua kinywa, amesema nini? Kwanini kaamua hivyo? Huyu hapa Nuh Mziwanda anafunguka katika sauti hapo chini.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top