Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WEWE NI MVUTAJI WA SHISHA?. HAYA HAPA MADHARA YAKE BAADA YA KUGUNDULIKA INAMADAWA HAYA YA KULEVYA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Wakati dunia nzima leo ikiadhimisha Siku ya Tumbaku Duniani, kwa upande wa serikali ya Tanzania i...
shisha
Wakati dunia nzima leo ikiadhimisha Siku ya Tumbaku Duniani, kwa upande wa serikali ya Tanzania iliarifu kuwa ipo katika hatua za mwisho za uchunguzi kuhusu shisha na itatoa tamko rasmi juu ya matumizi ya shisha katika sehemu za starehe na mikusanyiko ya watu.

Hayo ni kwa mujibu wa hotuba ya Aprili 30, 2016 bungeni ya Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.

Lakini nchini Kenya imekuwa tofauti baada ya Wizara ya Afya nchini humo kumaliza uchunguzi wake na kusema imebaini asilimia 80 ya Shisha inayovutwa nchini humo ina chembechembe za Madawa ya Kulevya aina ya Cocaine.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo kupitia mtandao wa Twitter, inasema katika kila kipimo cha shisha kati ya vitano vilivyojaribiwa waligundua kuwepo kwa chembechembe za dawa ya kulevya aina ya Cocaine licha ya kuwepo kwa madawa mengine pia.
shisha
Hata hivyo taarifa ya wizara hiyo imeeleza masikitiko yake kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushindwa kuitumia ipasavyo Siku ya Tumbaku Duniani kwa kuonya watu kuhusu madhara yatokanayo na uvutaji wa tumbaku.

Licha ya kupita ndani ya maji, moshi wa shisha huwa na kiwango kikubwa cha carbon monoxide na nicotine ambazo humfanya mtumiaji awe kwenye hatari kubwa ya Kupata Tatizo la Kansa ya koo, ama mapafu, Matatizo ya Moyo, Fangasi na Kifua Kikuu (TB), Kuzaa Njiti (mtoto mwenye uzito mdogo), “Nicotine Addiction”, Kupoteza Uwezo wa Kujamiiana, Kuchakaa kwa ngozi, Asthma na Allergy nyingine.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top