Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WAZIRI W AFYA ASITISHA ZOEZI LA UGAWAJI WA CHAKULA LILILOPANGWA KUANZA MUHIMBILI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa afya , Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametaka kusitishwa kwa z...
Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametaka kusitishwa kwa zoezi la ugawaji wa vyakula lililopangwa kuanza kutolewa kwa wagonjwa watakaolazwa katika hospitali ya Muhimbili kuanzia Julai 1 mwaka huu.
Ummy Mwalimu
Juni 21 uongozi wa hospitali ya taifa Muhimbili ulitangaza kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa hospitalini hapo kwa kuchangia kiasi cha shilingi 10,000 kwa ajili ya huduma hiyo pekee.

Waziri Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari ameagiza kusitishwa kwa muda zoezi hilo mpaka hapo wizara yake itakapopatiwa taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za utaratibu huo uliopangwa kutolewa hospitalini hapo.

“Wizara masikio tumesikia maoni na ushauri kutoka kwa wananchi, wengine wanaona utaratibu mzuri wengine wanaona ni mbaya. Lakini kubwa tunazidi kusisitiza kuwa Hospitali ya Taifa ipo wakati itabidi ibaki kama Hospitali ya Taifa, hata hii hudumu ilipendekezwa kwa ajili ya kuboresha huduma ila jambo hili limekuja kwa haraka sana,” alisema Ummy Mwalimu.

Aliongeza kuwa, “kufuatia hali hii kuleta wasiwasi kwa wananchi na wagonjwa, nimeagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kusitisha utaratibu huo mpaka hapo tutakapopata taarifa za kutosha kuhusu faida na hasara za utaratibu mpya unaopendekezwa. kwa hiyo nimeshatoa maelekezo hautaanza tujipange kwanza kwa mwezi mmoja au miwili.”

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top