Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WASANII WAITAKA SERIKALI KUHAKIKISHA BAJETI YAO YA SHILINGI BILIONI 3 INATEKELEZEKA KWA VITENDO
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya hapo juzi Waziri wa Fedha, Dkt Philip Mpango kutangaza serikali kuitengea sekta ya sanaa,...
Baada ya hapo juzi Waziri wa Fedha, Dkt Philip Mpango kutangaza serikali kuitengea sekta ya sanaa, ubunifu, utamaduni na michezo shilingi bilioni tatu, baadhi ya wasanii wameipongeza hatua hiyo ya serikali ikiwa ndiyo mwanzo huku wengine wakiitaka bajeti hiyo iwe ya vitendo na siyo maneno.
Waziri wa Fedha, Dkt Philip Mpango
Wakiongea kwa nyakati tofauti tofauti na gazeti la Mtanzania wasanii wa muziki na wadau pia akiwemo Mkubwa Fella alisema kuwa ni mara ya kwanza kwa serikali kutenga fedha ya usimamizi wa kazi za wasanii. Kikubwa kinachotakiwa uimarishwe ulinzi wa kazi za wasanii ili waweze kujipatia maendeleo kupitia kazi zao.

Naye Stara Thomas alisema, “Tumeangaliwa kwa jicho la huruma hivyo tujitambue na tuitumie vyema nafasi hii, pia upande wa wezi wa kazi zetu tutashukuru kama litafanyiwa kazi vizuri kwani wasanii wengi wamekuwa wakikata tamaa kutokana na kuibiwa kazi zao.”

Aidha Mfalme wa Rymes, Afande Sele ameiomba serikali kusimamia na kuhakikisha utekelezaji huo unakamilika na siyo maneno hewa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top