Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: TUNDU LISSU KITIKIA WITO WA POLISI, KAHOJIWA KWA MASAA 3 NA KULALA RUMANDE, KESHO MAHAKAMANI (+Audio)
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
June 28 2016 Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alifikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisut...
Tundu Lissu
June 28 2016 Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alifikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa ajili ya kujibu tuhuma za uchochezi kupitia gazeti la mawio kwenye habari yenye kichwa kinachosema ‘Zanzibar Machafuko yaja’ dhidi yake na wenzake watatu.

Nje ya mahakama hiyo Lissu alizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa kauli ambayo imewafanya polisi wamuite kwa ajili ya mahojiano, Lissu alisema….


"Nchi yetu inaingizwa kwenye giza nene na dikteta uchwara hatuwezi kuongozwa na mtu wa namna hiyo, hata kama kachaguliwa na kuwa Rais"

Mbunge huyo wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amehojiwa na polisi kwa saa tatu kutokana na kauli hiyo aliyoitoa jana nje ya mahakama ya Kisutu wakati akiongea na waandishi wa habari. hivyo Lissu atalala rumande leo kwa amri ya ZCO baada ya kukosa dhamana na atafikishwa mahakamani kesho.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top