Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: TUNDU LISSU APANDISHWA KIZIMBANI LEO MAHAKAMA YA KISUTU, AACHIWA KWA DHAMANA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Na. Mwene Said, Dar es Salaam. Tundu Lissu (48) amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi ikiw...
Na. Mwene Said, Dar es Salaam.
Tundu Lissu (48) amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi ikiwemo kudharaulisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tundu Lissu
Lissu alisomewa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Bernad Kongola akisaidiana na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Nassoro Katuga na Salum Mohammed.

Kongola alidai kuwa Juni 28, 2016 eneo la Mahakama ya Kisutu Ilala Dar es Salaam mshtakiwa kwa nia ya kushawishi na kudharaurisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tundu Lissu
Alinukuu maneno ya Lissu kwamba "Mamlaka ya Serikali mbovu ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikteta uchwara lazima apingwe kila sehemu kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene"

Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.

Upande wa jamhuri ulidai upelelezi umekamilika na uliomba tarehe ya kusikilizwa maelezo ya awali.
Tundu Lissu
Upande wa utetezi ukiongozwa na jopo la mawakili 11 akiwemo Michael Ngalo, Peter Kibatala na wenzao uliomba dhamana kwa mshtakiwa kwa kuwa ni mbunge atakuwa mwaminifu hataacha kufika mahakamani.

Hakimu Yongolo alisema mshtakiwa atakua nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya sh milioni 2. 

Lissu alitimiza masharti hayo na atasomewa maelezo ya awali Agosti 2, 2016.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top