Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: THABANI KAMUSOKO SASA NJIA NYEUPEE, TP MAZEMBE WAVUTIWA NAYE
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
TIMU ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imesema imevutiwa na kiungo ...
TIMU ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imesema imevutiwa na kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko.
Thabani Kamusoko
Yanga na TP Mazembe zilichuana juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) uliomalizika kwa Yanga kulala bao 1-0.

Makamu wa Rais wa TP Mazembe, Mario Kawel alisema Kamusoko alicheza vizuri na ni aina ya mchezaji ambaye anafahamu majukumu yake uwanjani.

Mchezaji pekee wa Yanga aliyemvutia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi yao ni Thabani Kamusoko.
“Mchezaji mzuri aliyenivutia ni yule mwenye rasta kichwani (Kamusoko), sijui anaitwa nani, lakini ndiye aliyecheza kiwango bora katika mchezo wetu, nina hakika anastahili kucheza kwetu," alisema Kawel.

Hata hivyo, alipoulizwa kama watafanya utaratibu wa kumsajili hivi sasa kwa kuzungumza na Yanga, alijibu kwa kuhoji: “Wataka kutusaidia ili iwe rahisi kumpata?”

Alisema suala la usajili ni mchakato mrefu, pia linahusisha kwanza klabu na hatimaye mchezaji kwa kuangalia maslahi zaidi, hivyo wao wamethibitisha ubora wake na kwamba kama watataka wamsajili sasa au baadaye, hilo hawezi kuzungumza.
“Ni mchezaji wa Yanga, ana mkataba na Yanga, mimi binafsi nimesema nimevutiwa naye natamani acheze kwetu, kwanza nitazungumza na kocha wetu kuona naye kama amevutiwa, ndipo tujipange,” alisema kiongozi huyo.

Naye kocha wa TP Mazembe, Mfaransa, Hubert Velud, alimsifu kiungo huyo na kusema ana vitu vyote muhimu anavyopaswa kuwa navyo mchezaji. “Ni mchezaji mzuri, sijui mkataba wake ukoje, lakini ningefurahi kujumuika naye kikosini kwangu,” alisema kocha huyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top