Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: TAMBWE AFUNGUKA YA MOYONI KUHUSU UJIO WA STRAIKA HUYU MPYA WA YANGA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe , amesema kuchezea timu kubwa kama Yanga kunahi...
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe, amesema kuchezea timu kubwa kama Yanga kunahitaji ujasiri mkubwa kutokana na usajili unaofanywa kila wakati.
Amissi Tambwe
Mshambuliaji Paul Nonga, ameomba kuondoka Yanga akiwa ameitumikia timu hiyo kwa miezi sita katika mkataba wa miaka miwili, tatizo kubwa likiwa ni kushindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza, licha ya kuonekana nyota kwenye timu alizotoka za Mbeya City na Mwadui FC.

Ujio wa mshambuliaji mpya kwenye kikosi cha Yanga, Mzambia Obrey Chirwa, unaonekana kutishia maisha ya Tambwe kwenye kikosi cha kocha Hans Pluijm, lakini mwenyewe amesema haitakuwa rahisi kama ambavyo watu wanadhani, kwani ataendelea kucheka na nyavu kama kawaida.

“Nitapambana uwanjani na kocha ndiye atakuwa na maamuzi, lakini nakubali Chirwa ni mchezaji mzuri ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na bado kijana, tusubiri kuona,” alisema Tambwe.
Amissi Tambwe
Mfungaji huyo bora wa msimu uliopita akiifungia Yanga mabao 21, alisema mbali ya kujivunia rekodi zake nzuri alizoziweka tangu alipoanza kuichezea timu hiyo misimu miwili iliyopita, lakini bado ataendelea kupambana uwanjani kupigania nafasi yake ili kuendelea kuitumikia timu hiyo, ambayo imeboresha kwa kiasi kikubwa maisha yake.

Alisema amekuwa na bahati kubwa akiwa Yanga, hivyo anaamini ataendelea kufanya vizuri na kumvutia Pluijm, katika safu ya ushambuliaji sambamba na Mzimbabwe Donald Ngoma, ambaye ameonekana kufanya vizuri katika msimu wake wa kwanza.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top