Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: RUBY AWACHANA YAMOTO BAND, NI KUHUSU YEYE KUTOONEKANA KWENYE VIDEO YA "SUU"
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Msanii Ruby ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa Yamoto Band unaofahamika kwa jina la '...
Msanii Ruby ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa Yamoto Band unaofahamika kwa jina la 'Suu' amefunguka na kupinga kauli iliyotolewa na maneja wa Yamoto Band, Mkubwa Fella kuwa yeye ana stress ndiyo maana alishindwa kutokea kwenye video.
Ruby
Akiongea na Planet bongo ya East Africa Radio Rubby amesema Yamoto Band hawakuona umuhimu wake kwenye video hiyo ndiyo maana waliweza kushoot video hiyo siku ambayo yeye alikuwa busy na mambo yake mengine, na kusema kutokana na wao kutaka video hiyo ifanyike ndani ya siku hiyo na kupinga wazo la kumsubiri kidogo inatosha kuonyesha kuwa hawakuona umuhimu wa yeye kuwepo kwenye video hiyo, kwani angekuwa na umuhimu wangeweza kumsubiri.

"Unajua siku ambayo wao walikuwa wakishoot video hiyo mimi nilikuwa na mambo yangu mengine hivyo nilikuwa busy, niliwaomba kama wanaweza wanisubiri kidogo nimalizane na hizo kazi zangu lakini wao wakafanya video hiyo. Hilo linatosha kuonyesha sikuwa na umuhimu kwani ningekuwa na umuhimu wangeweza kunisubiri, mimi sikukataa na nilikuwa na uhakika asilimia mia nitakuwepo kwenye video ile sema kwa kuwa walikuwa na haraka ndiyo maana imetokea hivyo." alisema Rubby

"Kiukweli mimi nimeumia sana maana Audio ile tumefanya muda mrefu na waliweza kusubiri mpaka tukakamilisha iwaje kwenye video washindwe kunisubiri, maana hii kazi tunasaidiana mimi niliwaambia niko busy nisubirini wangeweza kunisubiri tu kisha tukafanya video pamoja" aliongeza Rubby

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top