Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: RAIS MSTAAFU MWINYI ASIFIA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameyasifia mabasi ya mwendo kasi baada ya hapo jan...
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi ameyasifia mabasi ya mwendo kasi baada ya hapo jana kufanya ziara yake ya kutembelea mradi huo ulioanza mwezi May mwaka huu.
Ali Hassan Mwinyi
Ziara ya Mwinyi ilianzia kituo cha Morocco na kwenda mpaka stendi ya Gerezani, Kariakoo na baadaye alielekea stendi kuu ya Kivukoni kwa kukamilisha ziara yake hiyo. Rais Mwinyi alisema kuwa, “Usafiri huu ni mkombozi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida ya usafiri unaosababishwa na msongamano wa magari katika maeneo ya mjini.”

Aidha Mwinyi aliongeza kuwa amejionea ujuzi na uroda kama watu wanavyosema na amefurahia sana mazingira ya mabasi hayo kwa sababu yanaubora na hayana usumbufu wala msongamano.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuheshimu njia za mabasi hayo ili kuepusha ajali zisizokuwa za ulazima.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top