Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: PATA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA ALHAMISI YA LEO JUNI 9,2016
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Vardy:  Kwa mujibu wa James Olley ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la The Evening Standar...
Transfer news
Vardy: Kwa mujibu wa James Olley ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la The Evening Standard na aliye katika kambi ya England huko Ufaransa ni kwamba Jamie Vardy amewaambia wachezaji wenzake kuwa anataka kubakia Leicester City kwa msimu mmoja zaidi na ana asilimia 80 za kuitosa ofa ya Arsenal.(The Evening Standard)

Ibrahimovic: Kocha wa Sweden Erik Hamren amesema nahodha wa timu hiyo Zlatan Ibrahimovic,34, hataruhusiwa kuondoka kambini kwa ajili ya kwenda England kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester United na badala yake atapaswa kusubiri mpaka michuano ya Euro itakapokuwa imekwisha.(Daily Mirror)

Holding: Arsenal wameripotiwa kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili mlinzi wa kati wa Bolton Wanderers Rob Holding, 20, baada ya ofa yake ya tatu ya £1.5m kukubaliwa na miamba hiyo ya Reebok Stadium. Ofa za a wali za Arsenal zilizokataliwa ni zile za £750,000 na £1.2m.(Daily Mail)

Vrsaljko: Atletico Madrid iko hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mlinzi wa kulia wa Sassuolo, Mcroatia Sime Vrsaljko kwa ada ya €15m. Vrsaljko(24), anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne utakaomwingizia mshahara wa €2m kwa mwaka. 

Lichtsteiner: Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anataka kumfanya mlinzi wa kulia wa Juventus Mswisi Stephan Lichtsteiner(32) kuwa usajili wake wa kwanza. Lichtsteiner ambaye ameichezea Uswisi zaidi ya michezo 80 anataka kuihama Juventus ili kumpisha Dani Alves na aweza akapatikana kwa dau la £12m.(The Sun)

Flores: Espanyol imemtangaza aliyekuwa kocha wa zamani wa Watford Muhispania Quique Sanchez Flores kuwa kocha wake mpya. 

Darmian: Kocha wa Manchester United Mreno Jose Mourinho ameripotiwa kuwa tayari kumuuza mlinzi wa kulia wa klabu hiyo Muitaliano Matteo Darmian katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya. Habari zaidi zinasema licha ya Darmian(24), kucheza michezo 39 msimu uliopita lakini Mourinho hajashawishika kuwa nae msimu ujao.(Tuttosport)

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top