Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MREMBO PINKIETO:ASEMA DAIREKTA ALINIOMBA PENZI LANGU
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo ya filamu, jina la Gisela Joseph ‘Pinkieto’ litakuwa si geni kwak...
Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo ya filamu, jina la Gisela Joseph ‘Pinkieto’ litakuwa si geni kwako. Huyu alikuwa ni sekretari wa marehemu Steven Kanumba lakini pia msanii aliyeigiza kwenye filamu mbalimbali.Gisela Joseph ‘Pinkieto’
Gisela Joseph ‘Pinkieto’

Aidha Pinkieto amesema kuwa Kanumba alikuwa Mtu muhimu sana kwake hasa katika suala la Sanaa na kazi kwani kifo hicho kilimsababishia adhani zile ndoto zake ndio zimefika kikomo lakini alipambana na kuweza kuendelea na kazi hiyo.

Msanii huyo pia amesema kuwa ameweza kufanya kazi na msanii wa vichekesho nchini Masanja mkandamizaji mara baada ya kutoka katika ofisi ya Kanumba hii ikiwa ni baada ya kifo chake lakini hakuweza kudumu kwa mda mrefu kwani aliamua kujiajiri.
Gisela Joseph ‘Pinkieto’
Akizungumzia suala la Madirekta kuwataka kimapenzi kabla ya kupewa nafasi za kuigiza katika filamu hizo amesema Jambo hilo linamchukiza sana na hata yeye lilishamtokea na alimpa makavu dairekta huyo, ameongeza ya kuwa kufanya hivyo kunaiporomosha sanaa hiyo hivyo amewasihi wasanii wenzake kujitambua ilikuepukana na jambo hilo.

Akizungumzia Upande wa Mahusiano yake Pinkieto amesema kuwa hivi sasa ana mpenzi japo kuwa anapata usumbufu kutoka kwa wanaume wakware wanao msumbua lakini amesema anajiheshimu na kumheshimu mpenzi wake wa sasa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top