Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MKUU WA MKOA WA LINDI GODFREY ZAMBI AFUNGA MAGHALA YANAYONUNUA UFUTA CHINI YA BEI YA SHILINGI 2100
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewaagiza wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote...
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewaagiza wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kuzuia mara moja wafanyabiashara wanaonunua Ufuta chini ya Bei Elekezi ya Shilingi 2100 kwa kilo, lengo likiwa kumpa mkulima bei bora ya mazao yake.
 Godfrey Zambi
Agizo hilo limeambatana na kuzuia na kufunga Maghala mbalimbali wilayani Nachingwea na Ruangwa ambayo yalikuwa yakinunua zao hilo kwa bei ya shilingi 1600 na 1500 kwa Kilo.

Akiwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo, ikiwemo ile Ikiwemo inayotekelezwa na Mfuko wa Jamii Tasaf na utengezaji wa Madawati, Mkuu wa Mkoa huo amekuta baadhi ya vyama vya msingi vikinunua zao la Ufuta kwa ukiukwaji wa Agizo la Mkoa.

Kwa upande wao, baadhi ya wakulima wameonyesha kutoridhika na agizo hilo la Mkuu wa mkoa, kutokana na hali ngumu walizonazo, huku wengine wakipongeza hatua hiyo inayolenga kumfanya Mkulima auze zao hilo kwa tija.

Katika Ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo wa Lindi alifunga Maghala ya Kijiji Cha Nambalambala wilayani Nachingwea, Mbekenyera, Naunambe, Nangumbu na Nanganga Stesheni wilayani Ruangwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top