Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MIJI 3 AFRIKA YENYE MAISHA AGHALI, DAR IMETAJWA?
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kimataifa linalotoa orodha ya miji ku...
Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kimataifa linalotoa orodha ya miji kufuatia mfumo wa maisha katika miji yote duniani la Mercer tayari limesema licha ya Afrika kuwa na miji mingi yenye kuvutia lakini ni miji 3 pekee ndio yenye maisha aghali.
mji wa Luanda
Shirika hilo katika ripoti yake ya orodha ya miji yenye maisha ghali ya juu kwa wageni kote duniani, lililoitoa siku ya Jumatano wiki jana limeorodhesha mji wa Luanda wa nchini Angola uliokua umechukua nafasi ya kwanza kwa kipindi cha miaka 3 umepinduliwa na mji wa Hong Kong katika na fasi hiyo, na mji wa Kinshasa wa nchini DR Congo kuchukua na fasi ya 6 na mji wa N’Djamena wa nchini Chad kuchukua nafasi ya 9 katika orodha hiyo.

Ifahamike ya kwamba orodha hiyo hufanyika kila mwaka, ila kwa bahati mbaya Jiji la Dar es Salaam linalopatikana nchini Tanzania na majiji mengine hayakutajwa kabisa kulingana na gharama za maisha kwa wananchi wake kuonekana kuwa ni za kawaida kwa wageni.

Credit: trtworld

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top