Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MAMA JANETH MAGUFULI AWASILI MIKOA YA LINDI NA MTWARA KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZI.
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Jamhuri y...
Mama Janeth Magufuli
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi na Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa.
Mama Janeth Magufuli
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na kinamama waliojitokea kumpokea alipowasili Mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.
Godfrey Zambi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akimshukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kwa kuamua kufanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Salma Kikwete
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiongea kwa niaba ya kina mama waliojitokeza kumpokea Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli ambapo alimuahidi kuendelea kumuunga mkono kwenye shughuli zake na kumtaka kwenda mkoni humo mara kwa mara kwa ajili ya ziara za kikazi.Katikati mwenye pochi ya bluu ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa.
Salma Kikwete
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Ungo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi. Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
Salma Kikwete
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Kitenge Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa.
Salma Kikwete
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiwakabidhi zawadi ya mbuzi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kushoto) na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa (katikati).
Mama Janeth Magufuli
Mtoto Lulu Charles akimpa shada la maua Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipowasili Mkoani Mtwara.
Mama Janeth Magufuli
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali waliofika kumpokea alipowasili Masasi Mkoani Mtwara.
Mh. Halima Dendegu
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akimueleza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli utekelezaji wa mambo mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wake.

PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top