Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MAHARUSI WAPIGWA MARUFUKU KUPAKA SHEDO
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Gazeti la Mtanzania limeripoti kuwa waumini wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika kanisa Katoli...
Gazeti la Mtanzania limeripoti kuwa waumini wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika kanisa Katoliki Parokia ya Hananasif Kinondoni, jijini Dar es salaam wamepigwa marufuku kupaka rangi ya mdomo “lipstick” wakati wa ibada ya misa takatifu ya ndoa.

Gazeti hilo limeongeza kuwa uamuzi huo ulitangazwa juzi jioni na Paroko wa Parokia ya Hananasif Kinondoni jijini Dar es salaam Padri Gasper Mtengeti, wakati wa ibada ya misa ya kumwombea marehemu Rose Michael iliyofanyika kanisani hapo.

Aidha gazeti hilo limeongeza kuwa kutokana na hali hiyo Padri Mtengeti aliwataka wanawake waache kupaka rangi wakati wa misa takatifu ambapo alitoa sababu tatu zinazotokana na Liturijia ya Ekaristi Takatifu (utaratibuwa uendeshaji wa ibada) chini ya kanisa Katoliki.

Padri Mtengeti alieleza sababu hizo kuwakataza maharusi wa kike kujipaka rangi ya mdomo kuwa rangi hiyo inayopakwa huwa inasalia katika chombo kinachobeba divai ambayo kiimani kwa dhehebu hilo ni damu ya yesu kristu.

Sababu nyingine iliyoelezwa kupitia gazeti hilo ni pamoja na kuwa rangi ya mdomo huwa inachanganyika na damu ya Yesu wakati wanapokunywa kitendo ambacho si chema mbele za Mungu, sababu nyingine ni kuwa rangi hizo hubaki kwenye kitambaa cheupe kinachotumika kufuta kikombe cha hostia baada ya kuguswa na midomo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top