Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: JASPER MAKALA WA MCDI KILWA ATWAA TUZO NYINGINE HUKO USA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi wa MCDI, Jasper Makala (Kulia) Akipokea Tuzo ya ya Mwaka 2016 Utunzaji na Uhifadhi wa...
Jasper Makala
Mkurugenzi wa MCDI, Jasper Makala (Kulia) Akipokea Tuzo ya ya Mwaka 2016 Utunzaji na Uhifadhi wa Misitu toka kwa Dr Gary Knel Afisa Mtendaji Mkuu Geographic Society jana huko USA.
Jasper Makala
Jasper Makala Akikabidhi Tuzo ya Whitley Award Kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi hivi karibuni.


Na Abdulaziz Video, Lindi
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhifadhi mpingo na maendeleo (MCDI) Mr Makala Jasper Usiku wa jana huko Washington DC-USA Ameibuka Kidedea baada ya kushinda Tuzo ya mwaka 2016 iitwayo National Geographic Society/Buffett Award for Leadership in African Conservation, Tuzo hiyo ina thamani ya Dolla 25,000.

Jasper Makala
Mkurugenzi wa MCDI Yenye makao makuu yake Kilwa Masoko Mkoani Lindi ameiwakilisha vyema Africa na Tanzania Ambapo kwa Kushinda Tuzo hiyo.


Ushindi huo ni Baada ya Kuwashinda Washiriki wengine 30 Toka bara la Africa na Wenye Uwezo mkubwa na kufanya mchuano kuwa mkali sana. 

Ikumbukwe hii ni tuzo ya pili ndani ya miezi miwili ambapo Makala Jasper aliwania tuzo za Whitley huko nchini Uingereza ambapo pia alishinda tuzo hiyo ambayo ilikuwa na thamani ya Paundi £35, 000. ambazo ni sawa sawa na zaidi ya Milioni 100 za Pesa ya Kitanzania.

Ushindi huo unatokana na Mawasilisho ya Utunzaji Shirikishi na Uhifadhi wa Misitu.


*************************************

SHUHUDIA VIDEO YA HOTELI MPYA ISIYORUHUSU WATEJA NA WAHUDUMU WAKE KUVAA NGUO

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top