Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: HUKUMU YA PROF. LIPUMBA CUF HII HAPA, BAADA YA KUTAKA KUTENGUA UAMUZI WAKE WA KUJIUZURU UENYEKITI (+Audio)
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF Abdul Kambaya. Agosti 6 mwaka jana Chama cha Wananchi...
Abdul Kambaya.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF Abdul Kambaya.
Agosti 6 mwaka jana Chama cha Wananchi (CUF) kilitikisika baada ya aliyekuwa Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho Prof. Ibrahim Haruna Lipumba kujiuzulu nafasi hiyo kwa kile alichodai maazimio yaliyopitishwa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), (NLD, NCCR, CHADEMA na CUF) hayakutekelezwa.

Baada ya kimya cha muda mrefu zikaibuka figisufigisu zikidai kwamba Prof. Lipumba anampango wa kurejea katika nafasi yake ya Uenyekiti ambapo imedhihirika leo hii baada ya kumuandikia barua Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharid Hamad ambaye yupo nje ya nchi kwa sasa huku nafasi yake ikikaimiwa na Magdalena Sakaya.

Prof. Lipumba
Prof. Lipumba
Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Wananchi (CUF) kifungu namba 117-119 kinatoa uhuru kwa mwanachama yeyote halali kufanya anavyojisikia ilmradi asivunje katiba ya chama kama anavyosikika katika sauti hapo chini Msemaji wa chama hicho Abdul Kambaya akifafanua zaidi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top