Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: HII NDIO LIST YA WASANII WALIONG'ARISHWA NA MKONO WA RAYVANNY (+Audio)
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mafanikio hayaji bila ya kujituma, msanii Neyo kutoka Marekani anayefanya vizuri kwenye muziki ni...
Rayvanny
Mafanikio hayaji bila ya kujituma, msanii Neyo kutoka Marekani anayefanya vizuri kwenye muziki ni mmoja ya wasanii wa nchini humo waliojaliwa uimbaji na uandishi wa muziki, tofauti na kipato kinachotokana na uimbaji lakini msanii huyo pia anaingiza hela kwa uandishi wa mistari, hii inaonesha kuwa mtu mmoja anauwezo wa kufanya mambo tofauti lakini yote akayafanya kwa umakini.
Rayvanny and Diamond
Msanii Barnaba kutoka THT ni mwandishi mzuri wa mistari, tofauti na uimbaji wa muziki yeye anaandika ingawa ni maarufu zaidi kupitia sanaa ya uimbaji, tayari ameshawaandikia wasanii wengi kama Shilole, Linah, Amini na wengine wengi, pamoja na kuwaandikia wasanii tofauti Barnaba ameweza kuwa na mafanikio kutokana na sanaa yake.
Shetta
Chipukizi anayekuja kwa kasi katika uimbaji kutokana na sauti yake na upangiliaji wa mistari Rayvanny almaarufu kama Raymond wa WCB, ambaye yupo chini ya Lebo hiyo inayomilikiwa na Super Star wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amegeuka lulu kutokana na vipaji lukuki alivyojaaliwa, tofauti na uimbaji Ray yupo vizuri kwenye uandishi wa mistari.
Ambwene Yessaya
Bila kupepesa macho msanii huyu siku za hivi karibuni ataendelea kuwa mgodi unaotembea kutokana na ubunifu anaoendelea kuuonesha katika sanaa ya muziki, mbali na Raymond kutoa ngoma zake binafsi kali zilizobamba unafahamu ni ngoma zipi za malejendari zilizohit kupitia mkono wa Raymond? 

Huyu hapa Raymond mwenyewe anafunguka katika sauti hapo chini.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top