Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: G-NAKO AMEAMUA KUMWAGA UGALI KUHUSU UTATA WA VIDEO YA AROSTO NA NISHER
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Rapper wa kundi la Weusi , G-Nako amesema hawana tatizo na Nisher licha ya hivi karibuni kutofau...
Rapper wa kundi la Weusi, G-Nako amesema hawana tatizo na Nisher licha ya hivi karibuni kutofautiana kuhusiana na video ya wimbo Arosto.
G-Nako
Akiongea na kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka, G-Nako alisema pamoja na Nisher kuwatupia lawama kibao Instagram, wao wamechagua kutojibizana kwakuwa hayo ni mambo ya kike.

Amedai kuwa makubaliano ya awali ya video hiyo hayakufanyika kwenye mtandao hivyo hawana haja ya kulumbana mtandaoni baada ya kupishana na muongozaji huyo.

Warawara amedai kuwa video aliyoongoza Hanscana ndiyo wanayoitambua kama official na tayari wameituma kwenye TV za nje ambako wanasubiri tu ianze kuchezwa.

Nisher alimtuhumu G-Nako kuingia mitini baada ya kutumia takriban shilingi milioni nne kufanya video hiyo na kisha rapper huyo wa Weusi kudai hajaridhika na video hiyo.

Msikilize akiongea hapo chini.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top