Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: EURO 2016: POLAND YASONGA ROBO FAINALI KWA PENATI 5-4!
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
POLAND imeingia Robo Fainali ya EURO 2016 baada ya kuitoa Switzerland kwa Penati 5-4 kufuatia Sare ...
POLAND imeingia Robo Fainali ya EURO 2016 baada ya kuitoa Switzerland kwa Penati 5-4 kufuatia Sare ya 1-1 katika Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EURO 2016, iliyochezwa huko Stade Geoffroy Guichard Mjini St Etienne.
Poland
Poland ndio walitangulia kwa Bao la Dakika ya 39 la Jakub Blaszczykowski na Switzerland kusawazisha Dakika ya 82 kwa tikitaka ya Xherdan Shaqiri.

Mabao hayo yalidumu hadi Dakika 90 kumalizika na Dakika za Nyiongeza 30 hazikubadili kitu na ndipo ikaja Tombola ya Mikwaju ya Penati Tano Tano.
Switzerland
Poland walifunga Penati zao zote 5 lakini Switzerland walikosa Penati ya Pili iliyopigwa na Mchezaji Mpya wa Arsenal, Granit Xhaka.

Kwenye Robo Fainali, Poland watacheza na Mshindi kati ya Croatia na Portugal wanaocheza baadae Leo.

VIKOSI: Switzerland: Sommer, Lichtsteiner, Schar, Djourou, Rodriguez, Behrami, Xhaka, Shaqiri, Dzemaili, Mehmedi, Seferovic
Akiba: Hitz, Moubandje, Elvedi, von Bergen, Lang, Embolo, Frei, Zakaria, Fernandes, Tarashaj, Derdiyok, Burki.

Poland: Fabianski, Piszczek, Glik, Pazdan, Jedrzejczyk, Blaszczykowski, Krychowiak, Maczynski, Grosicki, Milik, Lewandowski
Akiba: Szczesny, Jodlowiec, Linetty, Stepinski, Wawrzyniak, Peszko, Salamon, Zielinski, Starzynski, Boruc.

REFA: Mark Clattenburg (England)

MATOKEO YA JUMAMOSI JUNI 25
Switzerland 1 Poland 1 (Baada Dakika 120 1-1, Poland yasonga Penati 5-4)

Wales v Northern Ireland (1900, Parc des Princes, Paris)

Croatia v Portugal (2200, Stade Bollaert-Delelis, Lens)

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top