Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: DIAMOND AWAWEKA MASHABIKI NJIA PANDA BAADA YA KUTOA STATUS TATA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki, Diamond Platnumz ametoa kauli tata kuhusu uchawi na kuibua minong’ono mingi kat...
Msanii wa muziki, Diamond Platnumz ametoa kauli tata kuhusu uchawi na kuibua minong’ono mingi katika mitandao ya kijamii kuhusu wasanii kurogana.

Diamond Platnumz
Muimbaji huyo ambaye ana tuzo nyingi za kimataifa kuliko msanii yeyote nchini licha ya kukosa tuzo ya BET na kwenda kwa Black Coffee wa Afrika Kusini , alipost ujumbe wa ujio wa kazi yake mpya aliyowashirikisha wasanii wa kundi la P Square wa Nigeria huku akiwataka wenzake kutoa taarifa kwa waganga wao.

“Haya ongeeni vizuri na waganga wenu, baada ya siku nne naachia mashine nyingine,” aliandika Diamond kupitia twitter.

Kauli hiyo ya uchawi ambayo amekuwa akirudia rudia mara kadhaa katika mazungumzo yake, imewafanya mashabiki wa muziki kuamini kumbe wasanii wanatumia ndumba katika muziki wao.

Juni 5 mwaka huu, Diamond wakati akimtambulisha Rich Mavoko WCB, aliwataka waandishi wa habari kuacha kuchochea migogoro ya wasanii ili waganga na wao wapumzike.

“Watu wanapogombana tunaleta vita katika sanaa, familia, tuwapumzishe waganga na wao wanachoka, tunapeleka hela za bure,” alisema Diamond huku akicheka.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top