Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: DIAMOND AITAMBULISHA KOLABO YAKE MPYA NA RAYMOND
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Diamond Platinumz kupitia akaunti yake ya Instagram amepost kuwa miongoni mwa ngoma anazopenda ku...
Diamond Platinumz kupitia akaunti yake ya Instagram amepost kuwa miongoni mwa ngoma anazopenda kusikiliza kwa sasa kwenye gari lake ni ile kolabo aliyofanya na Raymond ambayo hata hivyo amegoma kuitaja ni ngoma gani. 
Platinumz na Raymond
Lakini kwa post hiyo inaonyesha kuwa wawili hao wanaowakilisha lebo ya Wasafi Classic wanaandaa ngoma ambayo wataitoa hivi karibuni ambapo mashabiki wake wanaonekana kuisubiri kwa hamu wakitaka Diamond aiachie.
Platinumz post
Post hiyo kama inavyoonekana kwenye ukurasa wa Instagram wa Diamond.

Raymond a.k.a RayVanny kwasasa bado anatamba na kibao cha Natafuta Kiki ambacho amekiachia hivi karibuni baada ya kufanya vizuri kwa ile ngoma yake iliyomtambulisha kwenye game inayojulikana kwa jina la ‘Kwetu’.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top