Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: BINTI WA MIAKA 12 ABAKWA NA WANAUME 2
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Katika kuelekea katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa siku ya tarehe 1...
Katika kuelekea katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa siku ya tarehe 16/06/2016 kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ikisema kuwa “Ubakaji na Ulawiti kwa mtoto vinaepukika chukua hatua kumlinda mtoto.”
PICHA HII HAIHUSIANI NA HABARI HII

Hali hiyo imekuwa tofauti katika Manispaa ya Lindi kwani Leo hii Lindiyetu.com imepokea taarifa ya Kubakwa kwa Mtoto wa Miaka 12 mkazi wa Rupiani kata ya mwenge na Vijana wawili.

Mtoto huyo akiongea kwa masikitiko makubwa amesema kwamba alibakwa wakati alipokuwa akitoka dukani kununua nazi ambayo alitumwa na mama yake, alipokuwa akirudi nyumbani ndipo alikutana na wabakaji hao na kumfunika kiroba na kumfunga Kamba na kumtendea unyama huo.

Kufuatia tukio hilo Tayari polisi inamshikiria mtu mmoja ambaye inasemekana siku za mwanzo tayari alishawahi kulalamikiwa na mtoto huyo kuwa alikuwa akimtaka.

Unaweza msikiliza hapa Mtoto na Mama yake wakielezea Tukio zima.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top