Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: ASKARI WASIOWAPIGIA SALUTI WABUNGE KUKUMBWA NA ADHABU HII HAPA, IMESEMWA LEO BUNGENI (+VIDEO)
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Dodoma. Serikali imetangaza adhabu ya kuwakata mishahara na adhabu nyingine askari polisi wote n...
Bungeni Dodoma
Dodoma. Serikali imetangaza adhabu ya kuwakata mishahara na adhabu nyingine askari polisi wote nchini ambao hawatawapigia saluti wabunge wa Bunge la Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Agizo hilo limetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Umwagiliaji William Ole Nasha wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Ole Nasha amesema kumpigia saluti mbunge ni jambo la lazima kwa askari kwa kuwa lipo kwenye moja ya masharti yao, hivyo kutokufanya hivyo ni kushindwa kutii kiapo cha uaminifu wao.

Ole Nasha alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Fakharia Shomar Khamis (CCM) ambaye alitaka kujua ni adhabu kiasi gani atapewa askari ikiwa atashindwa kutoa saluti kwa mbunge.


TAZAMA VIDEO HAPA:

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top