Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: ALICHOKIFANYA KANUMBA NDICHO ALICHOFANYA KAJALA (+Audio)
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Inapendeza pale wapenzi wanapokuwa katika tasnia moja mathalani ya muziki kama ilivyo kwa Jay Z n...
Inapendeza pale wapenzi wanapokuwa katika tasnia moja mathalani ya muziki kama ilivyo kwa Jay Z na Beyonce ama ilivyokuwa kwa Rihanna na Chris Brown kwani husaidiana kwa ukaribu zaidi na kujengana kimuziki.
Kajala Masanja
Waswahili husema “ndege wafananao ndio wanaoruka pamoja”, kuna kila sababu na uwezo wa mtu kuingia kwenye fani ambayo mtu wake wa karibu au mpenzi wake amepelekea yeye kuingia kwenye hiyo fani, Diamond Platnumz wakati Wema Sepetu alipokuwa mpenzi wake waliwahi kupanda jukwaani na kuimba wimbo kwa pamoja ingawa Wema hakuwahi kujihusisha na muziki.

Msanii wa Bongo Movie Flora Mvungi yeye aliingia kwenye muziki baada ya kuingia kwenye mapenzi msanii wa muziki H Baba, lakini pia H baba naye alianza kujihusisha na masuala ya muvi baada ya kuwa na mahusiano na Frola Mvungi.
Kajala Masanja
Kajala Masanja ndiye aliyemfanya Quick Racka kuingia kwenye tasnia ya filamu kama ambavyo Steven Kanumba alivyomwingiza Wema kwenye tasnia ya filamu. Quick Racka amejaaliwa vipaji vingi ikiwemo uandishi wa mistari, uimbaji na hata uigizaji, kwa upande wake ameshindwa kumfanya mpenzi wake afuate nyayo za uimbaji.
Quick Racka
Nini sababu ya yeye kushindwa? Yeye aliwezaje kuingia kwenye muvi? msikilize katika sauti hapo chini akitiririka.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top