Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: YANGA YAKABIDHIWA MWALI, BAADA YA KUTOKA SARE NA NDANDA FC UWANJA WA TAIFA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Yanga SC leo wamevutwa shati na Ndanda FC baada ya kutoka saree y...
Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Yanga SC leo wamevutwa shati na Ndanda FC baada ya kutoka saree ya goli 2-2, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikombe
Katika mchezo wa leo ambao umetumika vilevile kuwakabidhi kombe mabingwa wa ligi kuu msimu huu yanga sc, ulianza taratibu, huku kila upande ukimpa nafasi mpinzani wake achezee mpira.

Hali ya mchezo ulibadilika katika dakika ya 20 na Yanga SC kuanza kutawala mchezo na kupeleka mashambulizi ya kiasi langoni mwa Ndanda FC lakini washambuliaji wa Yanga walishindwa kutumia nafasi hiyo.

Katika dakika ya 28 Juma Abduli alimchezea faulo Atupele Green katika eneo la hatari na mwamuzi kuamuru penati iliyotiwa kimiani na Omary Mponda katika dakika ya 29 na kuipa uongozi Ndanda FC.

Kuingia kwa goli hilo kuliongeza umakini na kasi ya mchezo, huku yanga wakijaribu kutengeneza nafasi za kufunga goli kabla ya Saimon Msuva kuisawazishia Yanga SC katika dakika ya 35 akimalizia kazi nzuri ya Donald Ngoma, Vicent Bosue, na Geofery Mwashiuya.

Yanga Bingwa
Katika dakika ya 40 Donald Ngoma aliiandikia Yanga SC goli la pili akimalizia kazi nzuri ya Haji Mwinyi na kuipleka Yanga mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-1.

Kipindi cha pili Yanga SC waliendelea na kasi yao huku wakitengeneza nafsi ambazo waliendelea kuzipoteza.

Katika dakika ya 80 Salum Minely akimalizia kazi ya Omary Mponda na kuisawazishia Ndanda FC na kupeleka mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.

MATOKEO YA MICHEZO YA LEO
MGAMBO JKT 1-0 JKT RUVU
NDANDA FC 2-2 YANGA SC

About Author

Advertisement

 
Top