Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: YANGA SC USO KWA USO NA TP MAZEMBE PAMOJA NA MWARABU MMOJA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Draw ya kupanga makundi mawili ya timu zitakazo chuana kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali ya komb...
Draw ya kupanga makundi mawili ya timu zitakazo chuana kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika imekamilika na kila timu imeshajua itachuana na klabu gani katika hatua hiyo ya nane bora.
CAF Makundi
Mabingwa wa Tanzania bara klabu ya Yanga imepangwa Group A ambapo itachuana na TP Mazembe (Congo DR), MO Bejaia (Ageria) na Medeama (Ghana).

Mo Bejaia ni timu pekee kutoka Kaskazini mwa Afrika huku timu tatu zikitoka katika maeneo mengine tofauti ya bara la Afrika.

Group B lina klabu za Kawkab Athletic, Futh Union Sports (Morocco), Etoile du Sahel (Tunisia) pamoja na Ahly Tripoli (Libya).

Kundi B linazikutanisha timu zote zinazotoka ukanda wa Kaskazini mwa Afrika (timu kutoka mataifa ya Kiarabu) na hiyo imetokana na timu tano za ukanda huo kufuzu hatua nane bora kati ya nane.

About Author

Advertisement

 
Top