Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) WAGOMA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambao ulitangazwa na Rais pamoja na makamu wao...
Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambao ulitangazwa na Rais pamoja na makamu wao wa serikali yao ya wanafunzi DARUSO unaendelea muda huu ndani ya chuo hicho ambapo wanafunzi wamekusanyika katika eneo maarufu la "Revolution square" kwa amani huku wakiimba nyimbo mbalimbali (kama sio juhudi zako Nyerere..., Sitasimama maovu yakitawala...., Vijana tusilale bado mapambano.... Alisema Nyerere vijana wote tumelegea sharti tuanze mchakamchaka....) Wamesikika wakiimba kwa hisia.

Wanafunzi hao wanadai fedha zao za kujikimu ambao kwa kawaida zinatakiwa kutolewa kila baada ya siku 60 na kwa sasa ni zaidi ya wiki mbili zimepita bila wanafunzi hao kupewa fedha za kujikimu kwa madai kuwa serikali haina fedha.

Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.

Tayari Jeshi la Polisi limeanza kuwasili ndani ya eneo la Chuo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top