Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WAJUE WANAOTOKA NA KUINGIA BARANI ULAYA, TETESI ZA USAJILI JIONI YA LEO
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Alaba:  Habari kutoka Ujerumani zinasema David Alaba, 23 angependa kujiunga na Barcelona ikiwa tu...
Tetesi za Usajili
Alaba: Habari kutoka Ujerumani zinasema David Alaba, 23 angependa kujiunga na Barcelona ikiwa tu ataahidiwa kuchezeshwa nafasi yake ya kiungo na siyo ulinzi wa kushoto kama anavyochezeshwa sasa na Bayern Munich.(Mundo Deportivo) 

Benitez: Kocha Rafa Benitez amehakikishiwa kubaki Newcastle United hata kama timu hiyo ya St.James Park itashuka daraja msimu huu.(Daily Mail ) 

Rogic: Arsenal imeripotiwa kuwa katika mpango wa kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Celtic Muaustralia Tom Rogic, 23 baada ya kuridhishwa na maendeleo yake. (Sydney Morning Herald) 

RVP & Nani: Nyota wawili wa Fenerbahce Robin van Persie na Luis Nani huenda wakahamia China baada ya habari kudai kuwa Shanghai Shenhua imewaandalia dau nono la usajili.(Sabah) 

Xhaka: Arsenal imeripotiwa kujiweka katika mazingira mazuri ya kumtwaa kiungo wa Borussia Monchengladbach Granit Xhaka, 23 baada ya kuongeza ofa yake mpaka kufikia €43 million (£33.8m).(Rheinische Post) 

Vardy: West Ham United wameandaa kitita cha £25m kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy. Katika kuhakikisha jambo hilo linatimia West Ham United pia imepanga kumpa Vardy mshahara wa £120,000 kwa wiki. (Daily Mail) 

Dembele: Matumaini ya Leicester City kumtwaa kinda Ousmane Dembele, 18 yamekwaa kisiki baada ya nyota huyo wa Rennes ya Ufaransa kusema kuwa havutiwi na mabingwa hao wa England. (The Mirror) 

Perez: Leceister City wameripotiwa kuwa wako njiani kuvunja rekodi ya usajili kwa kumsajili mshambuliaji wa Deportivo La Coruna Lucas Perez. Perez, 27 amefunga mabao 17 katika michezo 35 ya ligi ya La Liga. 

Nainggolan: AS Roma imeitupilia mbali ofa ya €30m toka Chelsea kwa ajili ya kiungo wake Mbelgiji Radja Nainggolan, 25. (Gazzetta dello Sport) 

Mazzarri: Watford itamteua Walter Mazzarri kuchukua nafasi ya kocha wake mkuu Quique Sanchez Flores anayejiandaa kutimka mwisho wa msimu.

Rodgers: Swansea City imeripotiwa kuwa inafikiria kuachana na mpango wa kutaka kumrudisha kocha wake wa zamani Brendan Rodgers na badala yake itampa mkataba mpya kocha wake wa sasa Francisco Guidolin.

Pellegirini: Kocha wa Manchester City Manuel Pellegirini atakubali kibarua cha kuinoa Everton ikiwa kocha wa sasa wa klabu hiyo Roberto Martinez atatimuliwa. 

Rulli: Liverpool wameripotiwa kuvutiwa na mlinda mlango wa Real Sociedad Geronimo Rulli.(Daily Express)

Varane: Manchester United imeripotiwa kuandaa kitita cha £25m kwa ajili ya kimsajili mlinzi asiye na nafasi katika klabu ya Real Madrid Mfaransa Raphael Varane, 23. (Daily Mirror)

Ranieri: Makamu Mwenyekiti wa Leicester City Aiyawatt Srivaddhanaprabha amesema klabu yake inataka kumpa mkataba mpya wa muda mrefu kocha wake Claudio Ranieri.

About Author

Advertisement

 
Top