Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: TRISS AWAPONDA MAPRODUCER WABOVU, ASEMA WENGI HAWANA MIPANGO ENDELEVU
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Muziki wa Kibongo kwa sasa umeweza kutoka nje ya nchi na kufanya vizuri, lakini maendeleo hayo ya...
Muziki wa Kibongo kwa sasa umeweza kutoka nje ya nchi na kufanya vizuri, lakini maendeleo hayo ya muziki kimataifa yanatokana na ubunifu mahiri wa wasanii na midundo ya watayarishaji, Triss ni moja ya watayarishaji wabunifu wa Bongo amefanya kazi kadhaa zikiwemo za msanii Belle 9 ikiwemo Sumu ya Penzi, Amerudi na Wanitamani na nyingine nyingi.
Triss
Triss kupitia XXL ya Clouds FM ameeleza kuwa watayarishaji wengi wa kibongo hawana mipango endelevu kwa maana ya mtu akishakuwa mtayarishaji na amepata programu (software) anatengeneza beat anaona ameshamaliza.

“Kutengeneza mdundo (beat) kuna vitu vingi sana vya kujifunza kutoka hapo, na ndio maana production nyingi za kibongo hazina ubora wengi wanafanya kazi kiujanja ujanja”

Bonyeza hapa chini kumsikiliza akifunguka zaidi.

About Author

Advertisement

 
Top