Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: SAKATA LA WANAFUNZI UDOM, WAPINZANI WASUSIA TENA BUNGE.!
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Wabunge wa vyama vya upinzani wametoka tena nje ya ukumbi wa bunge jioni hii baada ya Naibu Spik...
Bunge
Wabunge wa vyama vya upinzani wametoka tena nje ya ukumbi wa bunge jioni hii baada ya Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson kukataa hoja ya wapinzania hao iliyolitaka bunge kuacha kujadili mambo yaliyokuwa yakiendelea kulingana na ratiba badala yake kujadili suala la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kama hoja ya dharura.

Upinzani ilikitaka kiti cha Naibu Spika kuamuru kujadiliwa kwa suala la wanafunzi kama hoja ya dharura na kulichukulia uzito wa juu kwani wametimuliwa chuo, hawana pa kwenda na wanahangaika mitaani hivyo serikali itoe mwongozo namna gani itawasaidia vijana hao.

Baada ya Naibu Spika kukataa kujadiliwa kwa swala hilo kama hoja ya dharura, aliamuru shughuli za bunge ziendelee kama ilivyopangwa na badala yake suala hilo litajadiliwa baadaye jambo ambalo wapinzani hawakukubaliana nalo ndipo wakaamua kususia bunge na kutoka nje ya ukumbi.


MSIKILIZE MBUNGE GOODLUCK MLINDA AKIFAFANUA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top