Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: RAMADHANI CHOMBO ‘RENDONDO’ AWATUMIA SALAMU YOUNG AFRICANS
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo wa Mbeya City FC , Ramadhani Chombo ‘Rendondo’ ameionya timu ya Yanga ya jijini Dar Es S...
Kiungo wa Mbeya City FC, Ramadhani Chombo ‘Rendondo’ ameionya timu ya Yanga ya jijini Dar Es Salaam kuwa ijiandae vya kutosha itakapokwenda jijini Mbeya mwanzoni mwa juma lijalo kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mei 10 mwaka huu.
Ramadhani Chombo
Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo, Redondo aliyekosa michezo miwili ya awali kupisha majeraha ya mguu kabla ya kurejea na kuichezea City kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar aliweka wazi kuwa ana imani kubwa na kikosi cha sasa cha timu yake, hasa baada ya ujio kocha Kinnah Phiri aliyefanikiwa kuyaondosha ‘makandokando’ yote yaliyokuwa nasababisha timu kufanya vibaya kwenye michezo iliyopita.

Nadhani Yanga wanatakiwa wajiandae vizuri, wanakuja kukutana na kikosi cha City ambacho kiko kwenye wakati mzuri hivi sasa,hivyo wasitegemee mteremko,ujio wa kocha Phiri umeiimarisha zaidi timu yetu, ametupa muongozo mzuri na amefanya kazi kubwa kuweka timu sawa, hivyo hao wanaokuja wajue watakutana na upinzani mkali,timu yetu sasa inacheza tofauti sana na ilivyokuwa inacheza hapo mwanzo, alisema.

Akiendelea zaidi Redondo, aliyewahi kucheza kwa mafaniko kwenye timu za Ashanti, Simba na Azam Fc alisema kuwa anafahamu mchezo huu utakuwa mgumu pande zote kwa sababu kila timu inahitaji matokeo kulingana na hali ilivyo kwenye msimamo, Yanga ikitaka kujihakikishia ubingwa na City ikihitaji kujiweaka kwenye mazingira mazuri zaidi licha ya kuwepo kwa uhakika kuwa itasalia kwenye ligi .

Kuhusu majaaliwa yake kwenye kikosi cha City Redondo alisema kuwa anaimani kubwa atakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao, na kuweka wazi furaha yake ya kuwa mchezaji wa timu hii tangu alipojounga nayo mapema mwezi Januari.

“Nilijiunga na City mapema mwezi januari, nakumbuka ilikuwa ni wakati wa usajiri wa dirisha dogo, binafsi nina furaha hapa na nitaka kufanya kazi zaidi na kwa uwezo wangu wote kwa sababu lengo langu ni kuendelea kuwepo, kwa ngumi mimi hii ni timu nzuri kuliko zote nilizowahi kucheza, kuna wakati najiuliza kwa nini sikuwa huku mapema lakini hii ni soka na maisha ya mchezo huu ndiyo yalivyo” alimaliza

Tangu alipojumuishwa kwenye kikosi cha City, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, amecheza mechi 8 na kufunga mabao 2, huku pia akiwa na rekodi ya kadi 2 za njano hadi sasa.

About Author

Advertisement

 
Top