Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: RAIS MAGUFULI ATOA AGIZO HILI KWA MIFUKO YA JAMII NCHINI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Rais John Magufuli ameiagiza mifuko ya hifadhi ya jamii kuacha tabia ya kujenga vitega uchumi vy...
Rais John Magufuli
Rais John Magufuli ameiagiza mifuko ya hifadhi ya jamii kuacha tabia ya kujenga vitega uchumi vya majengo makubwa yanayokodishwa kwa fedha nyingi ambayo hayawasaidii wananchi wa kawaida badala yake waweke vitega uchumi vitakavyo saidia kutengeneza ajira kwa wananchi hasa vijana wanaoteseka kwa kukosa ajira ya uhakika.

Rais John Magufuli ametoa kauli hiyo jijiji Arusha katika ufunguzi wa majengo mawili mapya ya kitega uchumi ya mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF yaliyo gharimu zaidi ya shilingi bilioni sitini ambazo amesema zingitumika kwenye kujenga vitega uchumi vingine vingeajiri watanzania wengi kuliko ilivyo kwa majengo haya.

Awali wakizungumzia uwekezaji huo wakurugenzi wa mfuko wa NSSF na PPF walitoa maelezo mafupi ya ghalama zilizo tumika na fedha zitakazo zalishwa baada ya kupata wapangaji katika majengo hayo.

Katika tukio ilo viongozi wawakilishi wa vyama vya siasa pia walipata nafasi ya kutoa salam zao ambapo msemaji mkuu wa CCM Christopher Ole Sendeka na Meya wa jijij la Arusha kupitia Chadema Calist Lazaro waliwakilisha vyama vyao.

About Author

Advertisement

 
Top