Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: RAIS MAGUFULI AAMUA KUFANYA HIVI YA SAKATA LA SUKARI KUENDELEA KUWAUMIZA WANANCHI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Serikali ya Tanzania imeagiza sukari ili kukabiliana na upungufu wa sukari uliopo nchini. Rais wa...
Serikali ya Tanzania imeagiza sukari ili kukabiliana na upungufu wa sukari uliopo nchini.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema badala ya kuwapa wafanyabiashara leseni ya kuagiza sukari kutoka ng’ambo, serikali yenyewe ndio itaagiza sukari hiyo moja kwa moja.

Kauli hiyo imekuja baada ya mabohari mengi kugundulika yakiwa yamejaa sukari iliyoagizwa kutoka nje na ile iliyonunuliwa kwa wingi kutoka kwenye kampuni za kusaga sukari za Tanzania.
“Kuna mmoja ambaye amepatikana Arusha amehodhi zaidi ya tani elfu tano ya sukari naye mwengine huko Kilombero amenunua sukari yote kutoka kwa kampuni za humu humu nchini na akaficha.” Alisema Magufuli

“Lakini hili ni swala la sasa tu, katika siku zijazo sukari itapatikana kwa wingi hapa Tanzania. Serikali imekwisha agiza sukari lakini hatutawapa hawa waliofilisi watanzania leseni ya kuingiza tena sukari. Serikali imeagiza na itauza sukari hiyo kwa bei ya chini, hilo ndilo lengo la serikali ” aliongeza Rais Magufuli huku mawananchi wakimshangilia.

Rais Magufuli imesadifiana na tangazo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa imeanza kugawa sukari iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria na kufichwa katika mabohari kote nchini.

TRA ilichukua hatua hiyo baada ya mwekezaji wa kibinafsi mkoani Lindi kupatikana na zaidi ya mifuko elfu tano za sukari kutoka nga’mbo.

About Author

Advertisement

 
Top