Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MAREHEMU PAPA WEMBA APEWA NISHANI YA HESHIMA NA RAIS KABILA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa JAMHURI YA WATU WA CONGO JOSEPH KABILA leo ametoa nishani maalum ya heshima kwa mwanamzik...
PAPA WEMBA
Rais wa JAMHURI YA WATU WA CONGO JOSEPH KABILA leo ametoa nishani maalum ya heshima kwa mwanamziki nguli wa nchi hiyo PAPA WEMBA aliefariki dunia jumapili iliyopita nchini Ivory coast wakati akitumbuiza.

Tuzo hiyo ameitoa katika ukumbi wa BUNGE LA nchi hiyo uliopo kwenye mji mkuu wa KINSHASA ambako mwili wa mwanamziki huyo umeagwa kwa heshima maalum ya serikali na wabunge.

Siku ya jumanne hapo kesho mwili wa PAPA WEMBA utapelekwa kwenye eneo la matongee eneo ambalo aliishi akiwa mtoto na wananchi watapata nafasi ya kuuga na kuzikwa siku ya jumatano hapo hapo jijini KINSHASA.

About Author

Advertisement

 
Top