Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: MAKAMU WA RAIS AWATAKA WANANCHI KUWAFICHUA WALA RUSHWA BILA YA KUWAONEA HURUMA.
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassani amesema madhara ya rushwa yakitokea katika jamii yoyot...
Mh. Samia Suluhu Hassani
Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassani amesema madhara ya rushwa yakitokea katika jamii yoyote hayabagui yanamdhuru kila mtu katika jamii husika na hivyo ameitaka jamiii kuhakisha kuwa inawafichua wala rushwa wote bila ya kuwaonea huruma kwani serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kupiga vita rushwa.

Mh Suluhu ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampeni ya longa nasi ambayo inatoa fursa kwa wananchi kutumia mitandamo mbalimbali ya simu kutoa taarifa mbalimbali zinazohusina na rushwa.

Naye waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejinment ya utumishi wa umma na utawala bora Mh Angela Kairuki ameitaka Taasisi ya Kuzuia na na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kuongeza kasi katika utendaji kazi wake ila ifanye kazi bila ya kumuonea mtu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola amesema wananchi wanaruhusiwa kupiga simu bure Kupitia namba 113 katika mitandao yote ya simu za mikononi na tarifa zao zitapokelewa na kufanyiwa kazi kwa umakni mkubwa kabisa.

Baadhi ya wananchi waliokuwa katika uzinduzi huo wamezungumza namna watakovyonufaika na mfumo huo huku Jakson Mmbando mwakilishi wa makampuni ya simu yeye akitokea Airtel akisema wamejipanga vyema kuhakisha kuwa wananchi wanatumia huduma hiyo bure ili kuweza kutoa taarifa zao kwa urahisi.

About Author

Advertisement

 
Top