Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: BILL NAS ATEMANA NA RADA ENTERTAINMENT YA TID, AJIUNGA NA LABLE HII HAPA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Mkali wa Ligi Ndogo na Hit Maker wa Chafu Pozi , Bill Nas ameachana na management yake ya zamani...
Mkali wa Ligi Ndogo na Hit Maker wa Chafu Pozi, Bill Nas ameachana na management yake ya zamani Rada Entertainment ambayo inamilikiwa na TID na kujiunga na label mpya itwayo ‘LFLG’.
Bill Nas
Akizungumza na Lindiyetu.com Ijumaa hii, Bill Nas amesema yeye na Rada kwa sasa wamebaki kama washikaji.

“Rada sijaondoka ila mkataba wangu mimi na Rada uliisha kwa sababu ulikuwa wa mwaka mmoja, tena uliisha muda mrefu toka mwaka jana mwezi wa 12. Kwa hiyo kwa sasa nipo kama familia tu na TID mimi ni kaka yangu, ni mtu ambaye ana mchango mkubwa kwenye sanaa yangu, kwa hiyo always tupo pamoja, lakini kibiashara nipo ndani ya label ya ‘LFLG’, hii ndio label ambayo nafanya nayo kazi, hata Chafu Pozi, audio na video nimeziandaa nikiwa kwenye label mpya,” alisema Nas.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa Chafu Pozi, amesema ana inaimani atafanya vizuri zaidi ndani ya label hiyo mpya kutokana na ushirikiano uliyopo ndani ya label hiyo.

About Author

Advertisement

 
Top