Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: AFYA:: KWA WANAUME NA WANAWAKE HII INAWAKUHUSU, SOMA HAPA
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Hadithi hadith, hadithi njoo uongo njoo utamu kolea. Hapo zamani za kale, kulikuwa na wapenzi walio...
Hadithi hadith, hadithi njoo uongo njoo utamu kolea. Hapo zamani za kale, kulikuwa na wapenzi waliopendana. Yani wale mahaba kisheti sio wale wa kupigana mitama vilabuni.
Condom
Haya siku moja bi dada kapita kituo cha afya kakuta mkutano unazungumzia kinga, muhudumu anafundisha matumizi ya Condom. Akiwa anafundisha, akawa kaivalisha kwenye kidole gumba jinsi inavyovaliwa. Mama wa watu kafurahi mwenyewe, kajibebea kibox huyooo hadi home.

Fast forward mabusu busu na kushikana kushikana, baadae bonge moja la mechi, chaga mbili tatu zimeshavunjwa hapo…wameloa majasho mama anaanza kumcheka mume. Mume leo nimekuweza ujue? Mume nini? Mama anaonyesha Condom imevalishwa kidoleni. Watu woyoooooo!

Sasa, kila siku nawahimiza kutumia CONDOM kwa kila tendo, leo ningependa kuwapa somo kidogo la matumizi sahihi ya Condom za kiume. Maana unaweza kuwa nayo afu ndio ikawa kama hiyo story hapo juu. Fuata hatua hizi basi.

Hakikisha umeangalia muda wa matumizi kwenye pakti ya Condom. Kama mda wake (expiry date) wa matumizi umekwisha basi haikufai.

Fungua kipakiti chenye kondomu wakati tu ukiwa tayari kuitumia. Bila hivyo yale mafuta mafuta maalum kwenye kondomu yatakauka. Unapofungua pakiti kuwa mwangalifu usiipasue, au kuitoboa wala kuiharibu kondom yenyewe. Ikipasuka itupilie mbali na uchukue nyingine (ndio maana unakuta tatu kwenye pakti ya Jero…yaani Mia tano tu)

Condom huwa zimesokotwa na kuwa kama duara. Wakati wa kuivaa, ile sehemu ya mafuta mafuta inapaswa kuwa nje. Hivyo basi ivae kwa kuikunjua kuanzia kwenye ncha (kichwa)cha uume. Minya sehemu ya chuchu ya kondomu kwa kutumia dole gumba na kidole chako cha kwanza ili kutoa hewa kutoka sehemu hiyo, ili manii yahifadhiwe mahali hapo pale yatakapotoka. Sasa Endelea kuishikilia kondom kwa mkono mmoja. Kwa kutumia mkono wa pili ikunjue hadi kufikia kwenye mavuzi yaani kwenye shina la uume. Kama mtumiaji hajatahiriwa anapaswa kuvuta lile govi la uume wake kabla ya kuvaa kondomu.

Condom zina mafuta ya kutosha, usiongeze mafuta mengine yoyote. Baada ya kufanya mapenzi condom inapaswa kuvuliwa kwa njia sahihi pia. Baada tu ya kufika kilele na kutoa manii, mwanaume anapaswa kuutoa uume wake kutoka ukeni, kabla haujalegea kabisa, kwani akichelewa huenda kondom ikatumbukia ukeni mwa mwanamke.

Shika Condom shinani mwa uume na kuivua taratibu pasi na manii kumwagika. Unaweza kuifunga kondom kwenye karatasi na kuitupa kwenye choo cha shimo. Usitupe kondom kwenye choo cha kupiga maji kwani huenda ikatatiza utendaji kazi wa choo hicho. Usitupe mahali ambapo watoto wataweza kuifikia. 

Tumia kondom nyingine kwa kila tendo jengine la kujamiana. Tumia Condom kila wakati unapofanya mapenzi.

About Author

Advertisement

 
Top