Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: ZITTO KABWE AWASHANGAA WAPINZANI KWA KUTOMSAPOTI RAIS MAGUFULI NA KUTOKA BUNGENI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa chama cha ACT Wazalendo umeelezea kuridhishwa na namna rais Dkt John Magufuli la kupam...
Uongozi wa chama cha ACT Wazalendo umeelezea kuridhishwa na namna rais Dkt John Magufuli la kupambana na vitewndo vya rushwa na ufisadi huku ukionekana pia kukosoa namna wabunge wa upinzani walivyotoka nje ya bunge.
Zitto Kabwe
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema miongoni mwa maeneo ambayo rais anapaswa kuyafatilia kwa karibu ni pamoja na mabilioni ya fedha yanayopotea kwakulipia mitambo ya kufua umeme ya IPTL.

Kuhusu hati fungani inayohusu dola milioni 600, ambazo zimeifanya serikali kuanza kulipa deni la tirioni 1.2, linalozidi kuongeza thamani katika deni la taifa, ambalo hadi kufikia mwaka 2020 serikali itakuwa imekwisha kulipa bila riba zaidi ya tirioni 1.8, kiongozi huyo wa ACT anazungumza.

Miongoni mwa masuala yaliyowafanya wapinzani kukacha vikao vya bunge la bajeti mjini Dodoma ni pamoja na bunge kutokurushwa moja kwa moja, matumizi ya serikali nje ya bajeti iliyopitishwa na bunge ikiwa ni pamoja na mawaziri wa serikali kutokuwa na miongozo ya utendaji kazi zao.

Kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa jimbo la Kigoma mjini amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa halimashauri kuu ya chama hicho, ambapo mwenyekiti wa chama hicho amesema kwa miaka mitano ijayo watakuwa wakijinasibisha kwa kauli mbiu isemayo siasa ni maendeleo.

About Author

Advertisement

 
Top